TARATIBU ZA KUTUMA NAKALA MAHALI POPOTE:
Wapenzi
wateja tunapenda kuwajulisha kuwa, tumeanzisha mfumo mpya wa utumaji wa Nakala
(Document) mbalimbali. Mfumo huu unajulikana kwa jina la QDT (Quick Document
Transfer). Mfumo huu unafanya kazi kama
ilivyo huduma ya FAX na huduma nyinginezo, isipokuwa
tumeboresha huduma hii. Utaweza kupata nakala zako (Document) sehemu yoyote,
kupitia mtandao wetu wa www.jamessabbicomputerclass.blogsport.com.Ukurasa
wa website yetu utakapoufungua utatazama katika kipengele kitakacho someka kwa
jina (QDT DATA RECEIVE) sehemu ya juu kulia. Nakala zako
utazipata mahali popote pale ilimradi utumie kompyuta iliyounganishwa na
mtandao wa Internet. Jinsi ya
kupata Nakala zako (Document). Fungua website yetu kisha fungua sehemu iliyoandikwa QDT DATA RECEIVE.
Kopi kazi zako, hamishia katika MS Word Program kisha Print.
Utaratibu wa kutuma, fika ofisini kwetu na lipia gharama za kazi unazotaka kutuma, kisha acha
ofisini kwetu namba ya simu ya mtu unayetaka kumtumia nakala hizo. Sehemu hiyo
itafichwa na kutokuonekana mara tu baada ya kuingizwa nakala za mteja wetu.
Mhusika atapigiwa simu na kujulishwa kuwa nakala ziko tayari katika mtandao.
Mteja atakayepokea nakala atapigiwa simu na atatoa muda ambao atakuwa katika mtandao (Internet), kisha
atatupigia tena simu kutujulisha turuhusu nakala zake (document) aweze kuzichukua. Mteja mara tu baada ya kuchukua nakala zake, ukurasa utafungwa
tena muda huo huo na kufutwa nakala hizo zote. Huduma hii ni rahisi na
itakufikishia nakala zako sehemu yoyote na kwa muda muhafaka.
Karibuni nyote na
Asanteni sana
0 comments:
Post a Comment